Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 09:39

Benin:Upinzani warejea bungeni baada ya miaka minne


Waangalizi na wanachama wa tume ya uchaguzi wakithibitisha idadi ya waliopiga kura katika uchaguzi wa bunge, kwenye kituo kimoja cha kupigia kura mjini Cotonou, Januari 8, 2023.
Waangalizi na wanachama wa tume ya uchaguzi wakithibitisha idadi ya waliopiga kura katika uchaguzi wa bunge, kwenye kituo kimoja cha kupigia kura mjini Cotonou, Januari 8, 2023.

Upinzani nchi Benin umerejea bungeni baada ya kutokuwepo kwa miaka minne, ukishinda viti 28 katika uchaguzi ambapo washirika wa Rais Patrice Talon walipata viti vingi, kulingana na matokeo ya awali yaliyotangazwa Jumatano.

Uchaguzi wa Jumapili ulikuwa mtihani kwa taifa hilo la Afrika Magharibi ambapo Talon alikuza maendeleo, lakini wakosoaji wanasema program yake ilidhoofisha demokrasia ya Benin ya vyama vingi iliyowahi kunawiri.

Chama kikuu cha upinzani cha Wademocrat kilishinda viti 28 huku muungano wa Republican (BR) na vyama shirika vya Talon Progressive Union for Renewal (UP-R) kwa pamoja vikipata viti 81, tume ya uchaguzi (CENA) imesema.

Matokeo ya mwisho ya bunge hilo lenye viti 109 yanatarajiwa kutangazwa Ijumaa baada ya uchaguzi uliofanyika kwa amani na kwa kufuata kanuni, kulingana na waangalizi wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Uchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS).

XS
SM
MD
LG