Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 26, 2022 Local time: 15:40

Bemba arejea DRC


Jean Pierre Bemba

Baada ya kukaa nje ya nchi kwa miaka 11 akiwa gerezani, Uholanzi makamu wa rais wa zamani wa DRC, Jean Pierre Bemba, amerejea nchini, Jumatano, hatua ambayo inaelezwa inaweza kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini humo.

Bemba mwenye umri wa miaka 55, ametangaza kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi uliocheleweshwa mara mbili na unaotarajiwa kufanyika hapo Disemba 23, 2018..

Aliwasili katika uwanja wa ndege wa Kinshasa kutokea Ubelgiji kwa ndege binafsi baada ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu – ICC kumuondolea mashtaka yake mwezi Juni.

Mara tu baada ya kuwasili, akiambatana na mke wake, kwenda kwenye chumba cha wageni mashuhuri cha uwanja wa ndege kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG