Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Agosti 17, 2022 Local time: 12:46

Bemba: Uchaguzi ujao DRC ni upuuzi


Aliyekuwa mbabe wa kivita nchini DRC Jean-Pierre Bemba.

Aliyekuwa mbabe wa kivita nchini DRC Jean Pierre Bemba Jumanne alidai kuwa uchaguzi uliocheleweshwa utakaofanyika  Desemba nchini humo ni mzaha tu baada ya mahakama ya katiba kumnyima nafasi ya kuwania urais.

Bemba ni miongoni mwa wagombea 6 walioondolewa kwenye orodha ya kugombania urais na tume ya uchaguzi kwenye zoezi hilo lililopangwa kufanyika decemba 23.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, wakati akifanya mahojiano na televisheni ya France 24, Bemba alisema ni jambo la kuhuzunisha kumuona rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akimtu akichagua ni nani watakaokuwa wapinzani wake.

Rais Joseph Kabila ambaye ametawala taifa hilo tangu 2001 hatimaye ametangaza kutowania urais kwa muhula mwingine baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu.

Hali ya taharuki na ghasia imeendelea kushuhudiwa kote nchini humo. Taifa hilo lililokuwa chini ya ukoloni wa Ubelgiji halijashuhudia mabadilishano ya amani ya madaraka tangu lilipojipatia uhuru mwaka wa 1960.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG