Milipuko ipatayo mitatu imetokea asubuhi ya Jumanne katika mji wa Brussels miwili katika uwanja wa ndege na mmoja katika kituo cha treni huku vyombo vya habari vikiripoti watu zaidi ya 20 wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Picha za video zilionyesha watu wakikimbia uwanja wa ndege wa Zaventem wakati milipuklo miwili ilipotokea saa mbili asubuhi na kupasua madirisha katika uwanja wa ndege na moshi ukifuka kuelekea anagani asubuhi.
Taarifa za vyombo vya habari zinaeleza kwamba mwendesha mashitaka mmoja wa Belgium amethibitisha shambulizi la kujitoa muhanga katika uwanja wa ndege wa Brussels.
Vyombo vya habari pia vimethibitisha kulikuwa na kelele katika lugha ya kiarabu kabla ya mabomu hayo kulipuka.
Nchi ya Belgium ipo katika tahadhari kubwa katika alama ya 4.
"Tunafuatilia ka karibu dakika kwa dakika " alisema waziri mkuu wa Belgium Charles Michel katika mtandao wa Tweeter.