Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 21:45

Bei ya mafuta nchini Kenya yapanda kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa


Magari yakiwa kwenye foleni kupata mafuta kwenye kituo cha mafuta cha Shell mjini Nairobi, Aprili 4, 2022.

Bei ya mafuta nchini Kenya Ijumaa imefikia kiwango cha juu kuwahi kushuhudiwa baada ya mamlaka ya nishati kurekebisha bei kwenye vituo vya mafuta, na kuzidisha ugumu wa maisha kwa mamilioni ya Wakenya.

Wakenya tayari wanakabiliwa na gharama kubwa ya maisha kutokana na kuongezeka kwa bei ya chakula, msururu wa kodi mpya na kushuka kwa shillingi.

Kwa bei hiyo mpya ambayo imeanza kutekelezwa leo na kuendelea kutekelezwa hadi Oktoba 14, bei ya lita moja ya petroli katika mji mkuu wa Nairobi imeongezeka kwa shilling 17 hadi shillingi 211.64, huku bei ya mafuta ya dizeli ikiwa shillingi 200.99 na mafuta ya ndege au kerosene ikiwa 202.61.

Waziri wa nishati Davis Chirchir amesema hali hiyo imesababishwa kwa kiasi kikubwa na hatua iliyochukuliwa mapema mwezi huu na Saudi Arabia na Russia, wazilashaji wakubwa wa mafuta duniani, kwa kupunguza uzalishaji wa bidhaa hiyo, hatua ambayo ilisababisha bei ya mafuta ghafi kupanda kwenye soko la kimataifa.

Forum

XS
SM
MD
LG