Bei za wastani za a mafuta nchini Marekani zimeshuka hadi chini ya dola 4 kufikia leo alhamisi, ikiwa ni mara ya kwanza katika muda wa miezi kadhaa, na kuwapa afueni kwa madereva nchini Marekani ambao ndiyo watumiaji wakubwa wa mafuta kote duniani.
Lita moja ya mafuta inauzwa dola 3.99.
Bei ya mafuta ilipanda na kufikia dola 5 mwezi Juni, kutokana na uvamizi wa Russia nchini Ukraine ulioanza mwezi februari.
Kwa kawaida, bei ya mafuta hupanda wakati wa joto na kupungua kipindi cha joto kikimalizika.
Wachambuzi wanasema kwamba huenda kushuka kwa bei ya mafuta kukamsaidia rais Joe Biden na chama chake cha democratic, katika uchaguzi wa katikati ya u muhula.
White house imekuwa ikichukua hatua kadhaa kuhakikisha kwamba bei ya mafuta inashuka.