Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 22:42

Bei kubwa za dawa Nigeria kumewafanya baadhi ya wagonjwa kugeukia tiba ya asili


Mgonjwa wa pumu akizungumza na mfamasia huko Lagos Desemba 11, 2023. Picha na REUTERS/Temilade Adelaja.
Mgonjwa wa pumu akizungumza na mfamasia huko Lagos Desemba 11, 2023. Picha na REUTERS/Temilade Adelaja.

Gharama za kubwa za baadhi ya dawa nchini Nigeria kiwango ambacho kimepanda takribani mara kumi katika miezi michache iliyopita, kimewalazimisha baadhi ya wagonjwa kupunguza dozi au kugeukia tiba asilia.

Maafisa wa sekta ya dawa wamesema kushuka kwa thamani ya Naira baada ya kuondolewa katika udhibiti wa sarafu mwezi Juni kumefanya bei za bidhaa mpya kupanda.

Wakati Sodiq Ajibade alipokuwa akitoka katika duka la dawa mjini Lagos alikuwa ameshika dawa za pumu, aina moja ya dawa hakuwa nayo mkononi mwake kwa sababu hana pesa za kuinunua.

“Nilikuwa nikinunua dawa nilizoandikiwa na daktari za aina tatu, lakini sasa nimepunguza na kununua mbili ambazo ni penicillin na aminophylline” alisema Ajibade.

Rais wa Jumuiya ya Famasia ya Nigeria Cyril Usifoh, amesema dawa nyingi zinatoka nje ya nchi wakati watengenezaji wa ndani wanategemea uagizaji wa malighafi za kutengenezea dawa kutoka nje.

Tangu mwezi Juni, Naira imepoteza nusu ya thamani yake, na kuongeza bei ya kila kitu kuanzia dawa za maumivu mpaka dawa za magonjwa sugu.

“Ninacho khofia hasa ni vitu kama dawa za kansa, dawa za kuzuia shinikizo la damu, dawa za kisukari. Bei zimepanda sana” alisema Usifoh.
Dawa ya pumu ya Seretide inayotengenezwa na kampuni ya GSK kwa mfano mwezi April ilikuwa ikigharimu Naira 8,000 lakini sasa katika maduka ya rejareja inauzwa kwa Naira 70,000. Bei za dawa za antibiotic kama vile augmentin zimepanda na kufikia Naira 25,000 kutoka Naira 4,500 mwezi Julai.

Waziri wa Afya wa Nigeria na Shirika la Taifa la Chakula pamoja na Utawala na Udhibiti wa dawa haukuweza kujibu maombi ya maoni.

Msemaji wa GSK amesema uhaba wa fedha za kigeni umeathiri uwezo wa GSK kusambaza dawa na chanjo katika masoko, na kusababisha kutoweka kwa dawa madukani.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG