Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 11:41

Basi la Delux laungua moto likiwa na watu zaidi ya 40 ndani


Ajali ya basi
Ajali ya basi

Watu 14 wamefariki dunia katika ajali ya basi la Delux na wengine 35 kujeruhiwa katika mkoa wa Pwani .

Watu 14 wamefariki dunia na wengine 35 wamejeruhiwa vibaya katika ajali ya basi la abiria lililokuwa linatoka Ubungo jijini Dar es salaam kwenda Dodoma. Ajali hiyo imetokea jumatatu majira ya saa tisa na nusu mchana katika eneo la Kongowe.

Basi hilo linalomilikiwa na kampuni ya Delux lilipinduka mara tatu baada ya tairi lake la mbele kupasuka na kusababisha basi hilo kutoka nje ya barabara na kuungua moto papo hapo.

Mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza amesema jumatano watatoa taarifa kamili ya majina ya waathirika na kati ya maiti hao 14 ni watano tu wanaoweza kutambulika waliobaki wameungua na kueketea kabisa.

Aidha kuhusu chanzo cha ajali hiyo mkuu huyo ameeleza kuwa gari hilo lilikuwa likisafiri katika mwendo wa kasi na lilikuwa likijaribu kupita gari jingine na akawa anakutana na gari jingine na kujaribu kukwepa ndipo dereva alipopoteza mwelekeo na kupinduka.

Dereva wa gari hilo hajajulikana alipo na amesema watajua kesho baada ya zoezi la kuoanisha majina ya abiria na orodha ya wasafiri. Ila kondakta wa gari hilo ni miongoni mwa walionusurika.

Naye kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Ernest Mangu amesema watu walifurika katika eneo la tukio kujaribu kutambua ndugu zao na kusaidia katika harakati za uokozi.

XS
SM
MD
LG