Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 18, 2024 Local time: 11:34

Bashir yupo tayari kwa matokeo ya Kusini


Panamanian workers stand atop sacks of sugar inside a container aboard a North Korean-flagged ship at the Manzanillo International container terminal on the coast of Colon City, Panama, July 16, 2013.
Panamanian workers stand atop sacks of sugar inside a container aboard a North Korean-flagged ship at the Manzanillo International container terminal on the coast of Colon City, Panama, July 16, 2013.

Rais wa Sudan Omar al-Bashir anasema yuko tayari kuisaidia Sudan Kusini kama eneo hilo litapiga kura ya kuwa taifa huru siku ya Jumapili kama inavyotarajiwa.

Katika ziara yake katika mji mkuu wa Sudan Kusini - Juba, Jumanne, bwana Bashir alisema serikali yake inataka Sudan kuwa moja lakini itakubaliana na matokeo, katika maneno yake kusheherekea kama kusini wanaamua kujitenga.

Pia alisema Sudan Kaskazini na Kusini wana ushirikiano wa pamoja na kwamba Khartoum inajitayarisha kuipa kusini msaada wowote wa kiufundi inaohitaji.
Bwana Bashir amerudia kusema kuwa atakubali kusini kuwa taifa huru, baada ya miezi kadhaa ya maneno ya kuchanganyana kutoka kwake na maafisa wengine katika chama tawala nchini Sudan.

Kusini inapiga kura ya maoni kuwa taifa huru siku ya Jumapili. Waandaaji walisema Jumatatu wamejiandaa kikamilifu kwa asilimia 100 ya upigaji kura. Walisema takribani watu milioni nne kiasi cha nusu ya wakazi wa kusini wamejiandikisha kupiga kura.

Afisa mmoja wa cheo cha juu katika tume ya kura ya maoni, Chan Reec, alisema upigaji kura utaendelea licha ya upungufu wa fedha zilizoahidiwa kutoka serikali ya Bashir.

Kura ya maoni ni sehemu muhimu ya mkataba wa amani wa mwaka 2005 ambao ulimaliza zaidi ya miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya Sudan kaskazini na kusini.

XS
SM
MD
LG