Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 11:54

Harakati za kumrejesha Rais Barrow Gambia zinaendelea


Majeshi ya Senegal yakiingia Ikulu ya Banjul, Gambia
Majeshi ya Senegal yakiingia Ikulu ya Banjul, Gambia

Majeshi ya kieneo Afrika Magharibi yameingia Jumapili katika mji mkuu wa Gambia, Banjul, ambako wamepokelewa kwa shangwe kubwa saa baada ya Yahya Jammeh kukimbilia Equatorial Guinea.

Majeshi hayo yanategemewa kuimarisha utulivu kwa ajili ya kumwezesha rais mpya wa nchi hiyo Adama Barrow kuchukua madaraka, ambaye awali alichukua hifadhi katika nchi jirani ya Senegal wakati Jammeh alipokataa kuachia madaraka.

Mshauri maalum wa rais Barrow, Mai Ahmad Fatty amesema :“Ni kitu muhimu kabisa kwamba amani, usalama na utulivu wa nchi uhakikishwe upo.

Hali ya kisiasa na usalama iliyokwamisha demokrasia ambayo ililazimishwa juu yetu baada ya ushindi wa wazi katika uchaguzi wa Desemba 1, 2016, inaendelea kutoa changamoto na ugumu fulani katika ngazi zote na ni tatizo la msingi kabisa.”

Rais mpya wa Gambia Adama Barrow akiongea na mwandishi wa VOA Sainey Marenah, Senegal.
Rais mpya wa Gambia Adama Barrow akiongea na mwandishi wa VOA Sainey Marenah, Senegal.

Pia amedai kuwa Jammeh ameiba kwenye akaunti za serikali kutoka mabenki katika siku za mwisho za utawala wake.

Mshauri wa Barrow amesema: “Katika kipindi cha wiki mbili peke yake, takriban zaidi ya dolla milioni 11 zilitolewa kutoka mabenki na rais huyo wa zamani. Hicho ni kiwango kikubwa cha fedha, ukizingatia kuwa tunatumia (zaidi ya dola milioni 4.5 katika matumizi muhimu yanayohusiana na malipo ya wafanyakazi na mengineyo.”

Barrow amethibitisha Jumapili kuwepo mpango wa kuunda tume ya ukweli na maridhiano ilikuweza kuangalia kwa kina zaidi tuhuma za ukiukaji wa haki za binadamu wakati wa utawala wa Jammeh, ulianza mwaka 1994 mara tu baada ya mapinduzi ambayo hayakuwa na umwagaji damu.

Wanaharakati wa haki za kibinadamu wamedai kuwa ukandamizaji huo ulihusisha watu kukamatwa pasipo kufuata sheria, mateso na mauaji ya wapinzani.

Hadi Jumapili jioni, Jammeh ameripotiwa kuwepo Equatorial Guinea ambayo sio mwanachama wa umoja wa usalama wa kieneo uliokuwa umeongoza mpango wa kuingilia kati kumtoa Jammeh.

XS
SM
MD
LG