Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:48

Baraza la usalama laweka azimio kwa Sudan Kusini


Balozi wa Marekani, Umoja wa Mataifa, Samantha Power.
Balozi wa Marekani, Umoja wa Mataifa, Samantha Power.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, limeiwekea Sudan Kusini, shindikizo kwa kupitisha azimio linalotayarisha taratibu za vikwazo.

Vitahusu watu wanaotaka kuvuruga utaratibu wa Amani na kuvunja haki za binadamu nchini humo.

Wanachama wote 15 wa baraza hilo walipigia kura kuwepo kwa kamati ambayo itakuwa na nguvu ya kupendekeza vikwazo.

Wale wote wanaodhaniwa kusababisha hali ya mzozo ama kuzuia kumalizika vita watawajibishwa.

Sudan Kusini, imekuwa katika miezi 15 ya mapigano iliyoua zaidi ya watu 10,000 na kukosesha makazi watu milioni 1.5 katika taifa hilo changa duniani.

Azimio hilo liliandaliwa na ujumbe wa Marekani ulioongozwa na balozi Samantha Power.

Power amesema vikwazo vya silaha vinawezekana endapo pande zinazopingana hazita heshimu mpango wa amani.

Mazungumzo baina ya serikali na waasi yanaendelea wiki hii nchini Ethiopia, Alhamisi ikiwa ni siku ya mwisho ya kufikia maafikiano.

XS
SM
MD
LG