Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 14:17

Baraza la usalama lapitisha azmio juu ya Abyei


Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa

Walinda amani wa Ethiopia kupelekwa Abyei

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio kuruhusu kupelekwa kwa walinda amani 4,200 katika eneo lenye mgogoro la Abyei lililopo katikati ya Sudan Kaskazini na Kusini.

Wanachama wote 15 wa Baraza la Usalama wamekubali walinda amani kutoka Ethiopia wapelekwe Abyei kwa miezi sita kwanza. Kupitishwa kwa azimio hilo kunafuatia makubaliano baina ya Sudan Kaskazini na Kusini yaliyofikiwa June 20 ambayo yalihimiza kuondolewa kwa majeshi ya pande hizo mbili huko Abyei na kuwekwa kwa jeshi la kulinda amani linalosimamiwa na Umoja wa Mataifa.

Azimio la jumatatu linasema kwamba majeshi hayo yatafuatilia na kuhakiki kuondoka kwa majeshi ya Sudan na vikosi vinavyoutii utawala wa Kusini, ambao wamekuwa wakipigana kwa wiki kadhaa sasa. Baada ya kumalizika kwa hatua hiyo, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, wanajeshi wote wataondolewa katika eneo hilo ispokuwa askari polisi wa Abyei.

XS
SM
MD
LG