Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 15:15

Baraza la usalama la UN lalaani marufuku kwa wanawake kusoma kwenye vyuo vikuu Afghanistan


Mkutano wa Baraza la usalama la Umoja wa mataifa kuhusu Haiti
Mkutano wa Baraza la usalama la Umoja wa mataifa kuhusu Haiti

Baraza la usalama la Umoja wa mataifa Jumanne limeomba wanawake na wasichana nchini Afghanistan washirikishwe kikamilifu na kwa usawa, likilaani marufuku kwa wanawake kusoma kwenye vyuo vikuu au kufanya kazi kwenye mashirika ya misaada ya kibinadamu, iliyowekwa na utawala unaoongozwa na Taliban.

Katika taarifa iliyokubaliwa kwa maafikiano, baraza hilo lenye wanachama 15 limesema marufuku kwa wanawake na wasichana kusoma kwenye shule za sekondari na vyuo vikuu nchini Afghanistan “inawakilisha mmomonyoko unaoongezeka wa kuheshimu haki za binadamu na misingi ya uhuru.”

Marufuku kwa wanawake kusoma kwenye vyuo vikuu ilitangazwa wiki iliyopita, wakati Baraza la usalama likikutana mjini New York kujadili hali ya Afghanistan.

Wasichana walipigwa marufuku kusoma kwenye shule za sekondari tangu mwezi Machi.

XS
SM
MD
LG