Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 18:10

Baraza la Usalama la UN kuitisha kikao nadra cha dharura cha Baraza Kuu


Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa (Picha na AP)
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa (Picha na AP)

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitarajiwa kupiga kura Jumapili kuitisha kikao nadra maalum cha dharura cha Baraza Kuu lenye nchini wanachama 193 wa umoja huo kuzungumzia uvamizi uliofanywa na Russia huko Ukraine, kikao kitafanyika Jumatatu, wanadiplomasia wamesema.

Kura zitakazopigwa na wanachama 15 wa baraza hilo ni utaratibu tu hivyo hakuna mwanachama wa kudumu kati ya watano wa baraza hilo – Russia, China, Ufaransa, Uingereza na Marekani – atatakiwa kutumia kura yake ya turufu. Hatua hiyo inahitaji kura tisa kuunga mkono, kuna uwezekano mkubwa kupita, wanadiplomasia wamesema.

Vikao 10 kama hivyo maalum vya dharura vya Baraza Kuu vimeitishwa tangu mwaka 1950. Ombi la kikao kuizungumzia Ukraine limekuja baada ya Russia kutumia kura ya turufu Ijumaa dhidi ya rasimu ya azimio la Baraza la Usalama la UN ambalo lingelaani uvamizi wa Moscow. China, India na UAE hazikupiga kura, wakati wanachama 11 waliosalia walipiga kura kuunga mkono azimio hilo.

Baraza Mkuu linatarajiwa kupiga kura kwa azimio kama hilo kufuatia taarifa za siku kadhaa zilizotolewa na nchi mbalimbali katika vikao maalum vya dharura, wanadiplomasia wamesema. Maazimio ya Baraza Kuu siyo amri lakini yana uzito wa kisiasa.

Marekani na washirika wake wanataka kupata uungaji mkono kadiri iwezekanavyo ili kuionyesha Russia kwamba imetengwa kimataifa.

Baraza Kuu la UN lilipitisha azimio Machi 2014 kufuatia kujiingiza kwa nguvu katika mkoa wa Crimea huko Ukraine. Azimio hilo, lilitangaza kuwa kura ya maoni kuhusu hadhi ya Crimea ilikuwa batili, ilipata kura za ndio 100 na kura za siyo 11. Darzeni mbili ya nchi hazikupiga kura na nchi 58 zilijiweka kando.

Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres amezungumza na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy Jumamosi, akimwambia chombo hicho cha dunian kimepanga kuimarisha misaada ya kibinadamu kwa ajili ya watu wa Ukraine,” msemaji wa UN alisema.

“Alimjulisha Rais kuwa UN itawasilisha Jumanne ombi la ufadhili wetu kwa ajili ya operesheni za kibinadamu nchini Ukraine,” msemaji wa UN alisema katika taarifa yake.

Mkuu wa misaada wa UN Martin Griffiths alisema Ijumaa kuwa zaidi ya d ola bilioni 1 zitahitajika kwa ajili ya operesheni za misaada huko Ukraine katika kipindi cha miezi mitatu ijayo wakati maelfu ya watu wakijaribu kuondoka nchini baada ya Russia kumvamia jirani yake.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG