Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 23:41

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kukutana kwa dharura


Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litafanya mkutano wa dharura Jumatano kujadili majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini yaliyorushwa kufika mpaka Japan.

Mkutano huo wa wazi umeitishwa na Marekani.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Linda Thomasa-Greenfield, amesema lazima waidhibiti Korea Kaskazini kuwa na uwezo wa kutengeneza makombora yake yaliyo kinyume cha sheria ya maangamizi ya umma.

Hirokazu Matsuno, katibu wa baraza la mawaziri la Japan, aliwaeleza wanahabari mapema Jumanne kwamba Korea Kaskazini ilirusha makombora majira ya saa moja na dakika 22 asubuhi ya Japan.

Makombora hayo yalidondokea katika bahari ya Pacific, nje ya eneo la kiuchumi la Japan dakika 22 baadaye.

Ilisababisha Tokyo kuondoa baadhi ya wakazi wa maeneo ya Kaskazini ya Kokkaido na Aomori, Jumanne Asubuhi.

XS
SM
MD
LG