Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 20, 2023 Local time: 19:50

Baraza la usalama la UM lataka misaada kwa Syria kuongezwa


Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wiki hii lilifikiria kuidhinisha kufunguliwa zaidi kwa vivuko vya mpakani upande wa kaskazini  magaharibi mwa Syria ili kuongeza kasi ya misaada ya kibinadamu kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Linda Thomas-Greenfield amesema katika taarifa yake ya Jumapili kwamba watu wa maeneo yaliyo athirika wanawategemea wao na kuomba ubinadamu wao ili kusaidia katika kipindi hiki cha mahitaji.

Ameongeza kusema kwamba hawawezi kuwaangusha waathirika na wanapaswa kupiga kura haraka kwa azimio kuutaka Umoja wa Mataifa kuidhinisha vivuko vya ziada vya mpakani kwa ajili upelekaji haraka wa misaada ya kibinadamu.

Nakuongeza kwamba wana uweo wa kuchukua hatua. Wakati umefika kufanya hivyo kwa uharaka zaidina lengo maalum.

Umoja wa Mataifa umekosolewa kwa kuwa na mwitikio wa taratibu wa kuwasaidia waathirika wa Syria kaskazini.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG