Baraza la usalama la umoja wa mataifa limegawanyika kuhusu namna Korea Kaskazini inavyoongeza vitendo vyake vya kiuchokozi vya majaribio ya makombora.
Hali hiyo ikiendelea, wapinzani wake Japan na Korea Kusini zinaendelea kukabiliana na upinzani nyumbani na nje ya nchi kwa kuendeleza sera zaidi za vitendo vya kijeshi.
Wanachama 15 wa baraza la usalama Jumatano walikutana baada ya maombi ya Japan na Marekani baada ya Korea Kaskazini kuzindua makombora mawili mapema ambayo yalitua ndani ama karibu na eneo la maji linalo milikiwa na Japan.
Balozi wa Japan katika umoja wa mataifa amewaambia wanahabari kwamba hali hiyo kwa hakika ni tatizo kubwa kwa ulinzi na usalama wa eneo hilo.