Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 14:16

Baraza la Seneti Rwanda lapitisha mabadiliko ya muhula wa urais


Bunge la Rwanda
Bunge la Rwanda

Baraza la seneti nchini Rwanda limepitisha mabadiliko mapya ya kipengele cha katiba kitakachomruhusu Rais Paul kagame kuendelea kubaki madarakani hadi mwaka 2034.

Uwamuzi huo ulichukuliwa kwa sauti moja siku ya Alhamis. Mabadiliko yaliyopendekezwa yatafikishwa mbele ya wananchi ili kuweza kupiga kura ya maoni ambayo inatarajiwa kupata ushindi kiurahisi.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame.
Rais wa Rwanda, Paul Kagame.

Rais Kagame mwenye umri wa miaka 58, ameiongoza nchi ya Rwanda tangu jeshi lake lilipomaliza mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 na kuwaondoa madarakani wahutu wenye msimamo mkali nchini humo. Chini ya sheria iliyopo hivi sasa, bwana Kagame anatakiwa kujiuzulu mwishoni mwa muhula wake wa pili madarakani mwaka 2017.

Lakini kipengele kilichopendekezwa kinamruhusu bwana Kagame kuwania muhula mwingine wa miaka saba madarakani, kisha ikifuatiwa na mihula miwili ya miaka mitano madarakani.

XS
SM
MD
LG