Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 25, 2024 Local time: 22:13

Baraza la seneti lamthibitisha Ketanji Brown kuwa jaji wa mahakama ya juu

Jaji Ketanji Brown Jackson katika kikao cha uthibitisho bungeni mjini Washington Dc.
Jaji Ketanji Brown Jackson katika kikao cha uthibitisho bungeni mjini Washington Dc.

Baraza  la Seneti la Marekani lilimthibitisha Jaji Ketanji Brown Jackson katika Mahakama ya Juu ya Marekani Alhamisi kwa kura 53-47, na kumfanya kuwa mwanamke wa kwanza mweusi  kuwa jaji katika mahakama ya juu zaidi nchini humo.

Makamu wa Rais Kamala Harris aliongoza wakati huo wa kihistoria, ingawa Wademokrat hawakuhitaji kura yake katika bnaraza la Seneti iliyogawanyika kwa usawa ili kumthibitisha Jackson.

Warepublican watatu Susan Collins, Lisa Murkowski na Mitt Romney wote walipiga kura kumuidhinisha jaji huyo mwenye umri wa miaka 51, jaji wa tatu pekee mweusi katika historia ya Mahakama ya Juu ya Marekani.

Katika kikao cha siku nne mbele ya Kamati ya Mahakama ya Seneti mwezi uliopita, Wanademokrat walimsifu Jackson kwa uzoefu wake wa kina, alihudumu kama jaji kwa karibu miaka 10 katika ngazi ya serikali kuu na rufaa, na karani wa jaji wa Mahakama ya Juu Stephen Breyer, ambaye Rais Joe Biden amemteua kuchukua nafasi yake.

Jackson anaungana na majaji wengine watatu wanawake katika mahakama hiyo Sotomayor, Kagan na Amy Coney Barrett ikiwa ni mara ya kwanza kwa mahakama hiyo kuwa na wanawake wanne kwa wakati mmoja.

XS
SM
MD
LG