Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 11, 2023 Local time: 04:18

Baraza la mahakama kesi ya Boston, Marathoni, lakamilika


Majeruhi wa mashambulizi ya Boston, Marathoni, ya mwaka 2013.

Baada ya miezi miwili ya kuchagua wajumbe wa baraza la mahakama, jopo la wajumbe 12, na wengine sita wa badala limekamilika Jimanne.

Jopo hilo ni kwa ajili ya kesi ya serikali kuu yenye hukumu ya kifo kutokana na shambulio la mbio za Marathoni mjini Boston, inayomkabili mtuhumiwa Dzhokhar Tsarnaev.

Baraza linajumuisha wanaume 8 na wanawake 10, akiwemo mpaka rangi wa nyumba aliyejiajiri, muongoza ndege, msaidizi wa juu wa kituo cha sheria, na muuguzi wa huduma za dharura.

Mwanzo wa kusoma mashtaka umepangwa kufanyika Jumatano.

Tsarnaev mwenye miaka 21 alisema hana hatia katika makosa 30 yanayomkabili ya kulipua mabomu mawili katika mstari wa kumalizikia mbio mwezi April 2013.

Mabomu hayo yaliua watu watatu na kujeruhi wengine zaidi 260.

Makosa hayo yanajumuisha kifo cha polisi wa chuo cha Teknolojia cha Massachusetts, baada ya shambulizi.

Makosa 17 kati ya 30 ni ya adhabu ya kifo.

XS
SM
MD
LG