Rasimu hiyo, iliyoandaliwa na Ukraine kwa kushauriana na washirika wake na kujadiliwa na nchi zinazoridhiana nayo, itapigiwa kura mwishoni mwa kikao maalum cha dharura cha Baraza hilo kitakachoanza Jumatano alasiri na kuendelea hadi Alhamisi.
Inasisitiza dharura ya kupata “amani ya haki na ya kudumu kulingana na kanuni za Mkataba wa Umoja wa mataifa” na kutoa wito kwa nchi wanachama wa Umoja wa mataifa na mashirika ya kimataifa kuunga mkono juhudi hizo.
“Nadhani inashangaza kwamba ina baadhi ya maneno kuhusu umuhimu wa amani kuliko baadhi ya maazimio ya awali, mkurugenzi wa shirika linalofuatilia migogoro kwenye Umoja wa mataifa International Crisis Group, Richard Gowan ameiambia VOA.
Azimio hilo linaomba pia usitishwaji wa mapigano na kuondoka kwa wanajeshi wa Russia kwenye ardhi ya Ukraine ndani ya mipaka yake inayotambulika kimataifa, kwa maneno mengine, yakiwemo maeneo ambayo Russia inadai kuwa imeyanyakuwa.
Facebook Forum