Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 18:35

Baraza kuu la bunge Misri lafanya mkutano wa kwanza.


Spika mpya wa bunge la Misri Saad el-Katatni wa chama cha Muslim Brotherhood akisalimu wabunge katika kikao chao cha kwanza.

Baraza kuu Misri lafanya mkutano wa kwanza na huku wabunge wakila kiapo.

Baraza kuu jipya la bunge la misri limefanya mkutano wake wa kwanza tangu upinzani mkubwa uliomuondoa madarakani rais wa kiimla Hosni Mubarak mwaka uliopita , huku wabunge wa kiislam wakiwa ndio walio wengi.

Mbunge mzee kuliko wote Mahmoud el Saqqah alikuwa mwenyekiti wa kikao cha ufunguzi ambacho kilianza kwa kipindi cha kukaa kimya kuwakumbuka mamia ya watu waliouwawa katika maandamano ya kuipinga serikali mwaka uliopita.

Wabunge wa Misri halafu walikula kiapo kwa zamu kuheshimu katiba na sheria.

XS
SM
MD
LG