Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 08:49

Baraza jipya la mawaziri Tanzania halina mabadiliko makubwa


Baraza jipya la mawaziri Tanzania halina mabadiliko makubwa
Baraza jipya la mawaziri Tanzania halina mabadiliko makubwa

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania ametangaza baraza lake jipya la mawaziri akisema kuwa hakuna mabadiliko makubwa katika idadi ya wizara na hata mawaziri wenyewe.

Wachambuzi wa kisiasa wanasema hawadhani kutakuwepo na mabadiliko makubwa katika sera ya serikali kutokana na hali kwamba mawaziri wengi ni wale wale waliokuwa katika serikali iliyotangulia.

Akizungumza na sauti ya Amerika juu ya baraza hilo mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salaam na mchambuzi wa kisiasa Dk. Bashiru Ally amesema ,“Mabadiliko ni makubwa katika sekta ya ardhi, miundo mbinu elimu na ofisi ya waziri mkuu na ofisi ya rais lakini pia inaonekana kwamba mawaziri wengi waliokuwa kwenye serikali iliyopita wamerejeshwa ingawa wengi wao wamebadilishwa sekta na kuwekwa sekta nyingine ” .

Katika sura mpya imeonekana kuwepo Profesa Anna Tibaijuka na akizungumzia kuhusu nafasi ya wanawake kwenye baraza hili, Dk. Ally ameelezea kuwa karibu sekta zote muhimu zinazohusu maendeleo ya kijamii na kiuchumi kuna ama mwanamke ambaye anayeongoza wizara au anakuwa naibu waziri.

Ikiwa ni mhula wa mwisho wa Rais Kikwete , Dk. Ally anasema itamlazimu apambane na ufisadi na kuporwa kwa rasilimali asili ya nchi ikiwa atataka kukumbukwa vyema na wananchi wa Tanzania.

XS
SM
MD
LG