Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 03:17

Baraza jipya la mawaziri laapishwa Malawi


Rais wa Malawi Lazarus Chakwera
Rais wa Malawi Lazarus Chakwera

Serikali mpya ya Malawi imeapishwa Jumapili, baada ya rais   Lazarus Chakwera kushangaza kwa kuwafuta kazi mawaziri saba wiki iliyopita kutokana na shutuma za rushwa.

Wakati wa sherehe za kuwaapisha, Chakwera aliwataka viongozi walio apishwa kutokubali zawadi ili kutoa upendeleo kwa mtu pamoja na kuweka wazi vitendo vyao ili kujiepusha na rushwa. Makundi ya kiraia na kidini yamekuwa yakitoa msukumo kwa rais kulifuta baraza lake baada ya idadi kadhaa ya mawaziri wake kupokea rushwa kutoka kwa wafanya-biashara matajiri ili wapewe zabuni.

Chakwera alichaguliwa mwaka 2020 baada ya kufanya kampeni ambayo ilikuwa ikipinga rushwa katika taifa hilo masikini la kusini mwa Afrika, na cha kushangaza aliwafuta kazi baraza lote lililokuwa na mawaziri 33. Hata hivyo wengi wao waliteuliwa tena siku mbili baadaye ambapo baraza jipya lina sura mpya mbili tu.

XS
SM
MD
LG