Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 13:58

Ban Ki- moon apongeza juhudi za Obama.


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban-Ki Moon akiwa na Rais Barack Obama kwenye ikulu ya White House.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban-Ki Moon akiwa na Rais Barack Obama kwenye ikulu ya White House.

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon Jumanne amemsifu rais wa Marekani Barack Obama kwa uongozi wenye ujasiri na maoni katika harakati za kuendeleza mpango wa kupunguza hewa chafu inayotokana na viwanda vya Marekani.

Wito wa Bw Obama wa kupunguza kiwango cha utoaji hewa chafu cha asilimia 32 chini ya viwango vya 2005 kufikia 2030 umepingwa na viwanda vikubwa vya Marekani vikisema ni kinyume cha sheria na kuwa gharama yake ni kubwa.

Baada ya kukutana na Bwana Obama katika ikulu ya White House, kiongozi huyo wa umoja wa mataifa amesema kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa anaunga mkono pendekezo la rais Obama tangu siku ya kwanza alipoingia ofisini.

Bw Obama amesema tishio la mazingira kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ni swala nyeti linaloikabili dunia.

Kiongozi huyo wa marekani amesema mkutano wa kujadili mazingira utakaofanyika Paris mwezi desemba lazima ufanikiwe.

XS
SM
MD
LG