Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 10:55

Ban Ki-Moon aonya Senegal kuachana na ghasia


Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon.

waandamanaji wazusha ghasia baada ya kuwarushia mawe polisi na kuchoma matairi .

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki- moon ametoa wito wa kuwepo na utulivu huko Senegal ambako polisi wa kutuliza ghasia wamepambana na waandamanaji wakitaka rais Abdoulaye Wade asigombee tena kipindi cha tatu cha urais.

Katika taarifa iliyotolewa Jumanne bwana Ban alisihi pande zote mbili kuachana na ghasia na kutafuta njia za amani kutatua mzozo wa uchaguzi.

Maelfu ya raia wa Senegal, wengi wakiwa vijana walifanya kile walichodai kuwa maandamano ya amani jana katika mji mkuu wa Dakar.

Lakini ulipoingia usiku waandamanaji walibadili mwenendo na kusababisha ghasia huku wanafunzi wakiwarushia mawe polisi na kuchoma moto matairi na ndipo polisi wa kutuliza ghasia walijibu mashambulizi hayo.

Mashahidi na maafisa wanasema mwanafunzi mmoja mwenye miaka 30 alikufa baada ya kukanyagwa na gari kubwa wakati wa maandamano.Polisi wamekanusha ajali hiyo kusababishwa na gari la polisi.

XS
SM
MD
LG