Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 08:47

Ban Ki Moon alaani shambulizi lililotokea Yemen


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amelaani shambulizi moja la anga lililofanywa na ushirika unaoongozwa na Saudi Arabia nchini Yemen ambalo limeuwa watu 10 siku ya Jumamosi.

Kundi la misaada la madaktari wasio na mipaka limesema shambulizi huko Haydan limepiga shule moja na kuwajeruhi watu 28 wengine na kwamba waathirika wote walikuwa kati ya umri wa miaka 8 hadi 15.

Kundi hilo linatoa wito kwa pande zinazopigana nchini yemen kuchukua hatua madhubuti za kuwalinda raia. Ushirika unaoongozwa na Saudi Arabia ulianza kampeni zake za anga mwezi Machi mwaka 2015 kumsaidia Rais wa Yemen, Abdu Rabu Mansour Hadi, ambaye serikali yake ilifukuzwa kutoka mji mkuu na waasi wa kihouthi.

HRW group
HRW group

Makundi ya haki za binadamu yanalaumu pande zote katika mzozo kwa manyanyaso hususan katika kushindwa kuwalinda raia. Juhudi za amani zinazoongozwa na Umoja wa Mataifa zimeshindwa kumaliza mapambano yanayoendelea huko.

Msemaji wa ushirika huo aliliambia shirika la habari la Ufaransa siku ya Jumapili kwamba mashambulizi yamepiga kambi ya mafunzo ya wa-Houthi na kwamba serikali ya Yemen ilithibitisha hakuna shule katika eneo.

XS
SM
MD
LG