Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 14:37

Ban Ki Moon alaani muungano wa waasi Sudan.


Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon .
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon .

Ban Ki Moon amelaani SRF ambao ni muungano wa kundi lenye nguvu la waasi linalotaka kuangusha serikali ya Omar al Bashir Sudan.

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, ban ki moon ametoa taarifa kulaani muungano wa waasi huko Sudan unaodai unalenga kuangusha serikali ya Rais Omar al-Bashir.

Bw. Ban alisema katika taarifa jana kuwa analaani kuanzishwa kwa Sudan Revolutionary Front SRF . Alitoa wito kwa pande zote kutotumia nguvu, na kwa Sudan na Sudan Kusini watowe tena ahadi ya kujadiliana juu ya kufikia makubaliano kuhusiana na masuala ambayo bado yana mvutano kati yao.

SRF ni muungano wa kundi la Darfur lenye nguvu la waasi la Justice and Equality Movement na matawi mawili ya kundi la Sudan Liberation Army. Pia inajumuisha kundi la SPLM Sudan People’s Liberation Movement- North tawi la kundi la waasi ambalo lilipigania upande wa kusini wakati wa vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe kati ya kusini na kaskazini.

XS
SM
MD
LG