Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 08:17

Ban Ki Moon aitaka Sudan Kusini kuondoka Heglig.


Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa awaonya Sudan na Sudan Kusini.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa awaonya Sudan na Sudan Kusini.

Sudan kusini na Sudan zaonywa kuhusu mashambulizi na uwezekano wa kurudi vitani tena.

Mkuu wa Umoja wa mataifa amesema Sudan Kusini kulikalia kimabavu eneo la uzalishaji mafuta la Heglig ni kinyume cha sheria na kukiuka utaifa wa nchi jirani ya Sudan.

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York alhamisi katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon aliwaomba Sudan Kusini kuondoa majeshi yao kwenye eneo hilo la mpakani lenye utajiri wa mafuta ambalo linadaiwa na nchi zote mbili.

Bw.Ban pia aliitaka Sudan kuacha kufanya mashambulizi na kupiga mabomu maeneo ya Sudan Kusini na kuondoka kutoka kwenye eneo lenye mzozo la Abyei.

XS
SM
MD
LG