Sudan Kusini inapunguza idadi ya wafanyakazi wa balozi zake duniani kote kwa sababu ya kusuasua kwa uchumi wake kulikotokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe iliyochukuwa miaka miwili.
Waziri wa mambo ya nje, Barnaba Marial Benjamin, amekanusha habari kwamba Sudan Kusini itafunga afisi zake 10 za balozi lakini ailikubali kwamba serikali yake imekuwa ikichelewa kulipia kodi kwa baadhi ya balozi zake.
Waziri huyo aliiambia VOA kwamba kinachofanyika sasa kutokana na hali mbaya ya uchumi ni kupunguza wafanyakazi katika balozi zake ili kupunguza gharama za uendeshaji.
Amesema kupunguzwa huko kwa wafanyakazi kutathiri shughuli za afisi ambazo zina wafanyakazi wengi, akiitaja moja wapo ni ubalozi wake mjini Cairo, Misri.