Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 06:47

Ubalozi wa Marekani nchini Somalia utumike kumaliza mzozo Somalia


Stephen Schwartz, Balozi wa Marekani nchini Somalia
Stephen Schwartz, Balozi wa Marekani nchini Somalia

Mwanadiplomasia kutoka Somalia amesema kuwa Marekani lazima itafute mbinu mpya za kuleta uthabiti nchini Somalia kufuatia uteuzi wa Balozi wa Marekani nchini humo baada ya zaidi ya miaka 25.

Abukar Arman, aliekuwa wakati mmoja mwakilishi maalum wa Somalia hapa Washington, amesema Jumatano kuwa Marekani imekuwa ikizembea katika kutumia “nguvu ya chini chini” kwenye juhudi za kusaidia Somalia kupata usalama na uthabiti wa kisiasa.

Arman amesema uteuzi wa Stephen Schwartz kama Balozi wa Marekani nchini Somalia ni wa kihistoria lakini akaongeza kuwa balozi huyo lazima atumie nafasi hiyo kushinikiza ufunguzi wa akaunti za benki za kutuma pesa kutoka Marekani, kama moja ya hatua za kwanza.

XS
SM
MD
LG