Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 23:09

Balozi Mwapachu ameipongeza EAC kuwa na maamuzi ya pamoja


عکس ارسالی از سیل گلستان. بیشترین آسیب به شهر آق قلا رسید و هفتاد درصد شهر زیر آب رفت. شهر آق قلا در شمال گرگان قرار دارد.<br />
&nbsp;
عکس ارسالی از سیل گلستان. بیشترین آسیب به شهر آق قلا رسید و هفتاد درصد شهر زیر آب رفت. شهر آق قلا در شمال گرگان قرار دارد.<br /> &nbsp;

Katibu mkuu wa zamani wa jumuiya ya Afrika mashariki-EAC balozi Juma Mwapachu alipongeza hatua ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo ya kuwa na maamuzi ya pamoja katika kushughulikia mkataba wa ushirikiano wa kibiashara baina ya EAC na Jumuiya ya Ulaya yaani EPA.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:06 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


Mkataba baina ya EAC na Umoja wa Ulaya- EU juu ya ushirikiano wa Kibiashara baina ya Afrika, Carribean na Pasifiki - EPA una lengo la kuruhusu bidhaa za nchi hizo kuingia kwenye soko la Ulaya bila vikwazo na vile vile bidhaa za Ulaya kuingia kwenye soko la EAC bila vikwazo.

Katika kikao Maalum cha 17 cha wakuu wa nchi wanachama wa EAC kilichokutana Alhamis jijini Dar es Salaam, Tanzania na kuongozwa na mwenyekiti wa jumuiya hiyo Rais wa Tanzania, John Magufuli, viongozi hao wameutaka umoja wa Ulaya kuwapatia fursa zaidi hadi Januari mwakani ili waweze kujadiliana zaidi juu ya namna ambavyo viwanda vya nchi wanachama na wakulima wake watakavyolindwa kupitia mkataba huo.

Miongoni mwa Masuala ambayo yametakiwa kupewa muda zaidi kuyajadili ni namna gani wakulima wa jumuiya ya EAC watakavyoweza kuuza bidhaa na sio mali ghafi kwenye soko la umoja wa Ulaya, Ushiriki wa Burundi kwenye mkataba wa EPA huku ambapo mwanachama huyo amewekewa vikwazo pamoja na kuwepo kwa kipengele kinachonyima uhuru wa nchi moja kujitoa iwapo itakuwa hairidhishwi na ushirikiano wa EPA.

Rais Magufuli wa Tanzania akihutubia kikao maalum cha viongozi wa EAC Dar es Salaam
Rais Magufuli wa Tanzania akihutubia kikao maalum cha viongozi wa EAC Dar es Salaam

Katika mahojiano maalum na VOA jijini Dar Es Salaam katibu mkuu huyo mstaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki balozi Juma Mwapachu alisema Tanzania kwa mfano ilikuwa na shauku ya kuelewa namna azma yake ya kuwa nchi ya viwanda inavyoweza kuathirika na utekelezaji wa mkataba huo

Hata hivyo alipongeza juhudi za mwenyekiti wa EAC Rais John Magufuli kuweza kushawishi nchi zote wanachama kupata muda wa kushughulikia mkataba huo wakati baadhi ya nchi kama Kenya ikiwa tayari imesaini mkataba huo huku nyingine kama Uganda na Rwanda ikisemekana nazo zimesharidhia.

Balozi Mwapachu alibainisha kwanini Kenya imekuwa mstari wa mbele katika kutaka kufikia makubaliano ya kibiashara na umoja wa ulaya. Umoja wa wa Ulaya na jumuiya ya Afrika mashariki zilianza mazungumzo juu ya mkataba wa EPA mwaka 2007 ambapo ilitarajiwa kwamba ifikapo oktoba Mosi mwaka huu nchi zote wanachama wa EAC ziwe zimeridhia na kusaini mkataba huo kwa ajili ya utekelezaji.

XS
SM
MD
LG