Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 23:18

Bakili Muluzi akana mashitaka


Rais wa zamani Malawi Bakili Muluzi
Rais wa zamani Malawi Bakili Muluzi

Rais wa zamani wa Malawi Bakili Muluzi amekana mashitaka 12 ya rushwa

Rais wa zamani wa Malawi Bakili Muluzi amekana mashitaka 12 ya rushwa kutokana na shutuma kwamba alichukua dola milioni 12 kwa matumizi yake binafsi .

Rais huyo wa zamani alikana mashitaka katika mahakama kuu ya Blantyre Jumanne, miaka minne baada ya mashitaka kutolewa dhidi yake.

Rais wa zamani wa Malawi Bakili Muluzi
Rais wa zamani wa Malawi Bakili Muluzi

Waendesha mashitaka wamemshutumu Bw. Muluzi kwa kuchukua fedha za misaada ya maendeleo kutoka Taiwan, Morocco, Libya na nchi nyingine.

Awali alishitakiwa kwa makosa 86 ya rushwa lakini mahakama ilifuta mengi ya makosa hayo.

Muluzi mwenye umri wa miaka 67 amesema ni mgonjwa mno kuweza kusimama kizimbani kujibu mashitaka hayo. Alisema wiki iliyopita kwamba alifanyiwa upasuaji mara tatu kwa matatizo ya uti wa mgongo.

XS
SM
MD
LG