Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 22, 2024 Local time: 15:03

Bajeti za Afrika Mashariki zawekeza katika kilimo


Huduma za afya ni mionogni mwa viapau mbele vya bajeti za nchi za Afrika Mashariki
Huduma za afya ni mionogni mwa viapau mbele vya bajeti za nchi za Afrika Mashariki

Mawaziri wa fedha wa nchi nne za Afrika Mashariki wapendekeza kuwekeza katika kilimo, elimu na miundombinu na kuhakikisha ukuwaji uchumi na kulinda watu maskini

Serikali za Kenya, Uganda, Tanzania, na Rwanda zilitangaza makadirio ya bajeti ya mwaka 2011/2012 bungeni jumatano zikijaribu kutafuta uwiano kati ya sera za kupendelea ukuwaji uchumi na kupunguza mzigo wa ughali wa maisha na kupanda kwa bei za vyakula kwa watu maskini.

Mwandishi wa VOA Nairobi, Mwai Gikonyo anaripoti Waziri wa Fedha Uhuru Kenyatta alisoma bajeti yake bila ya shamra shamra za kawaida kwa vile alikiuka maagizo ya katiba mpya na kuonywa na Spika wa bunge kwamba atalazimika kusoma taarifa ya bajeti bila ya utaratibu wa kawaida.

Bw. Kenyatta alitangaza bajeti yenye matumizi makubwa kuwahi kutokea huko Kenya akitenga dola bilioni 4.7 kwa ajili ya maendeleo.

Hata hivyo, mbunge wa Budalang'i, Ababu Namwamba, anasema bajeti ya Kenya ya mwaka huu haitosaidia kupunguza gharama za maisha kwa mwananchi wa kawaida.

Kwa Tanzania mwandishi wa Sauti ya Amerika Dinah Chahali anaripoti kwamba Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo,alitangaza huko Dodoma bajeti inayotilia mkazo kilimo na miundo mbinu kwa lengo la kupunguza makali ya maisha kwa wa Tanzania yanayotokana na kupanda kwa kasi bei ya vyakula na huduma.

Nchini Uganda wananchi huwenda wakaridhika na habari kwamba bei za vyakula msingi zimepungua katika bajeti iliyotangzwa mjini Kampala. Mwandishi wa Sauti ya Amerika Leylah Ndinda anaripoti kwamba mbali na kushushwa ushuru wa bei za bidhaa muhimu wakulima pia watapatiwa nafuu katika ushuru wa vifaa vya kilimo.

Rwanda ambayo kwa mara ya pili tangu kujiunga na Jumuia ya Afrika Mashariki ilitangaza pia makadirio ya bajeti yake Jumatano, na mwandishi wa Sauti ya Amerika Kigali, Sylvanus Karemera, anaripoti kwamba bajeti hiyo inaweka fedha zaidi kuimarisha elimu kilimo na maendeleo ya mawasiliano ya teknohama.

XS
SM
MD
LG