Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 31, 2023 Local time: 18:40

Papa awakaribisha Abbas na Peres Vatican


Kutoka (L)Mahmoud Abbas, Papa Francis, Shimon Peres na mkuu wa kanisa la ki-Orthodox wakiwa Vatican, June 8, 2014.
Rais wa Israel Shimon Perez na kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas walijumuika na Baba mtakatifu Francis siku ya Jumapili huko Vatican kwa sala ya kuombea amani huko Mashariki ya kati ambayo haijawahi kufanyika.

Viongozi hao watatu wakiungana na mkuu wa kanisa la ki- Orthodox wa Constatinople, Bartholomew, walisikilizaa dua kutoka katika dhehebu la wakristo, wayahudi na waislam zilizotolewa na makadinali, maimamu na wa-rabbai wa kiyahudi.

Mkutano huo uliodumu kwa saa mbili katika bustani ya Vatican ulijumuisha sala kutoka Agano la kale na jipya katika Biblia na Quran zilizosomwa katika lugha ya kiyahudi, kiarabu, kingereza na kitaliano.

Baba mtakatifu Francis kutoka Argentina baadae alimwambia bwana Abbas na bwana Peres kwamba “kupatikana amani kunahitaji ushujaa zaidi kuliko vita. Alifafanua ushujaa kama ni kuwa tayari kusema “ndio” kukutana na “hapana” kwa mgogoro.

Baba mtakatifu alitoa mwaliko wa ghafla kwa viongozi hao wawili mwezi uliopita ikiwa wiki kadhaa baada ya kuvunjika kwa duru ya mwisho ya mazungumzo ya amani ya Mashariki ya Kati.
XS
SM
MD
LG