Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 11:13

Baba mtakatifu amesema aliandika barua ya kujiuzulu mwaka 2013


Baba mtakatifu Fransis
Baba mtakatifu Fransis

Akizungumza na gazeti la Spanish ABC, Fransis alisema alitoa barua hiyo kwa kadinari Tarcisio Bertone ambaye wakati huo alikuwa katibu wa Vatican. Ameongeza kuwa ana matumaini hivi sasa barua yenye maelekezo ya maandishi iko kwa Kadinali Pietro Parolin aliyeshika wadhifa huo.

Fransis ambaye ametimiza umri wa miaka 86 Jumamosi, alifanyiwa upasuaji mwaka 2021 ili kurekebisha utumbo mwembamba na amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya goti ambayo kwa miezi kadhaa yalimsababisha kutumia kiti cha wagonjwa .

Hata hivyo hivi karibuni amekuwa akitumia fimbo zaidi badala ya kiti hicho kwa ajili ya kuzunguuka hadharani.

Alipoulizwa nini kitatokea endapo maswala ya afya au ajali vitamsababisha kushindwa kuendelea na kazi zake , na kama kunapaswa kuwa na sheria kwa matukio kama hayo , Fransis alijibu kiutendaji tayari kuna sheria.

Alisema “ Tayari nimetia saini kujiuzulu kwangu, akibainisha kwamba alifanya hivyo mapema katika nafasi hiyo ya upapa.” Katika maelezo yake ya zamani , Fransis aliwahi kupongeza uamuzi wa mtangulizi wake baba mtakatifu Benedict XVI kujiuzulu kwa sababu alihisi kutokana na umri mkubwa asingeweza kutekeleza vyema majukumu yake.

Sheria za kanisa katoliki zinataka kujiuzulu kwa baba mtakatifu kudhihirishwe na uhuru wake kama ilivyokuwa wakati wa Benedict alivyoushangaza ulimwengu alipotangaza kujiuzulu katika Mkutano wa makasisi huko Vatican Februari mwaka 2013.

XS
SM
MD
LG