Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 21:03

Serikali ya Bujumbura yaridhia azimio la UN kupeleka polisi nchini Burundi


Polisi wakifanya doria katika mitaa ya mjini Bujumbura kufuatia shambulizi la gruneti.Dazeni ya watu walijeruhiwa hapo Ferbuari 15.
Polisi wakifanya doria katika mitaa ya mjini Bujumbura kufuatia shambulizi la gruneti.Dazeni ya watu walijeruhiwa hapo Ferbuari 15.

Serikali ya Burundi imesema imepokea azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa 2279 ambalo linataka kupelekwa kwa kikosi cha Polisi wa Umoja wa Mataifa kufuatilia hali ya usalama nchini humo.

Azimio hilo lililopitishwa Ijumaa pia linazitaka pande zote kukana aina ghasia za aina yeyote na taarifa zenye kuchochea chuki. Imeisihi serikali ya Burundi kuhakikisha uhuru kwa wote na kuheshimu utawala wa kisheria.

Waziri wa mambo ya nje wa Burundi, Alain Nyamitwe, amesema serikali ya Rais Pierre Nkurunzinza siku zote imekuwa wazi kwa kuwepo kwa jumuiya ya kimataifa nchini Burundi na wanakubali kupelekwa nchini humo kwa Polisi wa Umoja wa Mataifa mradi tu sio wanajeshi wa Umoja wa Mataifa.

XS
SM
MD
LG