Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 16, 2025 Local time: 05:47

Austria yazuia shambulizi la kigaidi kwa wanao shiriki mapenzi ya jinsia moja


Serekali ya Austria, Jumapili imesema imezuia shambulizi ambalo lilipangwa kufanyika wakati wa gwaride la wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja maarufu kama Pride la Vienna.

Inaelezwa lilipangwa kutekelezwa na vijana watatu ambao wanadaiwa kuunga mkono kundi la Islamic State.

Mkuu wa idara ya upelelezi ya Austria aliwaambia waandishi wa habari kwamba washukiwa hao, wenye umri wa miaka 14, 17 na 20, walikamatwa saa moja kabla ya kuanza kwa gwaride la Jumamosi la Pride, ambalo lilihudhuriwa na karibu watu 300,000, radio ya taifa ya ORF iliripoti.

Omar Haijawi-Pirchner kutoka idara ya Usalama wa taifa na ujasusi amesema hakukuwa na hatari kwa washiriki wa gwaride wakati wote.

Kansela wa Austria, Karl Nehammer alitoa shukrani zake kwa wapelelezi kwa kuzuia shambulio hilo Vienna.

Kupitia ujumbe wa Twittr alisema “hii inaonyesha kwa mara nyingine hatupaswi kamwe kujitoa katika vita dhidi ya watu wenye itikadi kali."

Forum

XS
SM
MD
LG