Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 14, 2026 Local time: 22:52

Australia yatangaza kuongeza dola milioni 123.9 za msaada huko Ukraine

Mwanajeshi wa Australia akizungumza na wanajeshi wa Ukraine. Feb. 1, 2023. (AP).
Mwanajeshi wa Australia akizungumza na wanajeshi wa Ukraine. Feb. 1, 2023. (AP).

Australia imetangaza kuongeza dola milioni 123.9 za msaada wa Operesheni iitwayo Kudu  kwa Ukraine.

Chini ya makubaliano hayo, serikali ya Canberra itapeleka wanajeshi wa ziada kwa misheni inayoongozwa na Uingereza ambayo imekuwa ikitoa mafunzo kwa wanajeshi wa Ukraine nchini Uingereza.

Ni takriban miaka miwili tangu Russia ilipoivamia Ukraine.

Tangu Januari 2023, wanajeshi wa Australia wamesaidia kutoa mafunzo kwa wapiganaji wa kujitolea wa Ukraine zaidi ya 1,200 chini ya mpango unaoongozwa na Uingereza.

Operesheni Interflex ilianza Juni 2022 na inahusisha wakufunzi wa kijeshi kutoka mataifa kadhaa, pamoja na Canada, New Zealand na Norway. Hakuna askari wa Australia atakayeingia Ukraine.

Wanajeshi wa Ukraine hufundishwa mazoezi ya kutibu majeruhi katika uwanja wa vita, jinsi ya kutumia silaha na kuhusu hatua za kukabiliana na ufuatiliaji kutoka kwenye ndege zisizo na rubani.

Kuanzia mwaka ujao, Jeshi la Ulinzi la Australia, ADF, litatuma wataalamu wa ziada wa mafunzo ya kijeshi kusaidia vikosi vya Ukraine. Canberra itapeleka takriban wanajeshi 90 kwa mzunguko wa miezi mitatu, kutoka kwaenye kikosi cha sasa cha 70.

Balozi wa Ukraine nchini Australia, Vasyl Myroshn-ychenko, aliliambia Shirika la Utangazaji la Australia leo Alhamisi kwamba rasilimali za ziada zitaleta mabadiliko.

Forum

XS
SM
MD
LG