Serikali ya Australia ilisema Alhamisi kuwa chombo cha kudhibiti wahamiaji nchini kinashindwa kutekeleza wajibu wake.
Waziri wa Mambo ya Ndani Clare O”Neil aliwaambia waandishi wa habari mapungufu katika mfumo wa uhamiaji, ikiwemo upungufu wa wafanyakazi, umeruhusu magenge ya kihalifu ya kimataifa kuwasafirisha waathirika wa biashara hiyo haramu kuwaleta Australia kwa madai ya utapeli ya kutafuta hifadhi au visa za utalii ambazo inatakikana zikaguliwe na kufuatiliwa na serikali.
Magenge hayo baadae huwalazimisha waathirika hao kuingia katika ukahaba nchini Australia.
O’Neil ameiita hali hiyo “kuwa ni ulaghai wa kustaajabisha ambao umetendwa kwa watu wa Australia.”
Shirika la Kimataifa la Kazi, ILO, na wanaharakati wa haki za binadamu wanakadiria kuwa kuna watu 15,000 ambao wamewekwa katika mazingira yanayo fanana na utumwa nchini Australia.
Mbali na wanawake wanaolazimishwa katika ukahaba, wapo wanaolazimishwa kuolewa, na pia wanaofanya kazi katika viwanda, migahawa au usafishaji.
Serikali pia ilisema kuwa madai uongo ya kutafuta hifadhi yanawawezesha waombaji kubakia Australia kwa takriban muongo moja huku wakiwa na visa za muda kabla ya kesi zao kutatuliwa.
Programu mbalimbali za elimu ya kimataifa, ambayo wanafunzi wa kigeni wanakuja kusoma Australia pia imebainika kuwa ni eneo linalo saidia kuingiza wahamiaji haramu na utoaji wa visa feki.
O’Neil aliliambia Shirika la Utangazaji la Australia kuwa udanganyifu umeenea katika mfumo wa utoaji visa.
Ripoti ya mwandishi wa VOA Phil Mercer.
Forum