Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 12:55

Austin apongeza 'uhusiano imara' kati ya jeshi la Marekani na la Kenya


Waziri wa ulinzi wa Marekani Llyod Austin na mwenzake wa Kenya, Aden Duale na maafisa wengine wa jeshi la Kenya, baada ya kusainiwa mkataba wa ushirikiano kati ya nchi zao mbili kwenye sekta ya ulinzi, Septemba 25, 2023.
Waziri wa ulinzi wa Marekani Llyod Austin na mwenzake wa Kenya, Aden Duale na maafisa wengine wa jeshi la Kenya, baada ya kusainiwa mkataba wa ushirikiano kati ya nchi zao mbili kwenye sekta ya ulinzi, Septemba 25, 2023.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Llyod Austin Jumanne amepongeza kile alichokitaja kuwa “uhusiano imara kati ya jeshi la Marekani na la Kenya wakati alipokutana na wanajeshi wa nchi hizo mbili kwenye kambi ya Simba huko Manda Bay, nchini Kenya.

Austin amesema”Nyinyi ni mfano wa ushirikiano. Mnafanya kazi bega kwa bega kila siku, mkijaliana kila mmoja, mkisaidiana na mnafanyakazi kazi katika baadhi ya masuala muhimu ya usalama.”

Marekani na Kenya zilitia saini Jumatatu mkataba wa miaka mitano wa wa ulinzi wenye lengo la kuimarisha juhudi za kupambana na ugaidi Afrika Mashariki na kuunga mkono juhudi za Kenya kuongoza kikosi cha usalama nchini Haiti.

Austin amesema Marekani inaishukuru Kenya kwa uongozi wake katika kukabiliana na changamoto za kiusalama katika eneo na kwingineko duniani, ameishukuru nchi hiyo kwa kujitolea kuongoza kikosi cha kimataifa cha usalama kupambana na magenge ya kihalifu nchini Haiti.

Austin alisema utawala wa Biden utashirikiana na Bunge ili kupata ufadhili wa dola milioni 100 kwa tume hiyo, msaada ambao uliahidi wiki iliyopita kando ya mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa mataifa.

Forum

XS
SM
MD
LG