Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 14:00

Raia wa Somalia wauwawa na vikosi vya AMISOM


Wanajeshi wanaotumika kama vikosi vya Umoja wa Afrika nchini Somalia

Takriban raia 14 wakisomali waliuwawa na wengine 3 kujeruhiwa kufuatia mapambano baina ya wanajeshi wa Ethiopia na wapiganaji wa Al shabab huko kusini magharibi mwa Somalia jumapili.

Maafisa katika eneo la Bay wameshutumu wanajeshi wa Ethiopia kwa kuuwa kiholela baada ya mapambano na wapiganaji wa Al Shabab katika kijiji cha Wardinle, kilomita 30 magharibi mwa mji wa Baidoa.

Mwanasheria wakisomali Ibrahim Isak Yarow ambaye alitembelea kijiji hicho jana , aliiambia sauti ya Amreica kuwa alihesabu miili 13 ya raia walouwawa mahala hapo wakati mwengine alikufa akiwa njiani akielekea hospitali. Anasema waathirika wote walikuwa raia.

Anasema janga hilo lilitokea huko Wardninle.

Yarrow, naibu waziri wa zamani wa usalama ambaye anawakilisha eneo hilo, anasema aliwahoji wanavijiji walomwambia kuwa vikosi vya Ethiopia vilipita kijijini humo jumapili wakiwa wanawasaka Al shabab. Anasema wanajeshi waliwaambia wanavijiji kuwa wanaelekea eneo ambalo wanashuku Al Shabab huwenda wakawa wanajificha takriban kilomita 3 kutoka hapo.

Bw Yarrow anasema kuwa Al Shabab waliingia kijijini humo, haikuwa bayana iwapo walikuwa wanatafuta chakula au kama walitaka kuteka nyara watu. Anasema haiko bayana lakini waliwashambulia wanajeshi.

Anasema watu wote 14 walouwawa walikuwa wanaume baina ya umri wa miaka 40 hadi 80. Mmoja wa wale walouwawa ni chifu wa kijiji hicho Aden Barire .

Vikosi vya Ethiopia ambao pia wanahudumu kama walinda Amani wa AMISOM walihusika katika mapambanao hayo.

Yarrow anasema alitembeleakambi ya kijeshi ya Ethiopia katika kijiji karibu na hapo cha Awdinle na kukutana na makambada wao, akitafuta majibu. Anasema wanajeshi wa Ethiopia walimwambia kuwa walishambuliwa na kwamba mmoja wa wanajeshi wao aliuwawa na mwengine kujeruhiwa.

Yarrow anasema watu walouwawa ni wenyeji na sio Al shabab, anasema wanajeshi wa Ethiopia wanajukumu kubwa katika mauwaji yao.

Abdi Addow mkuu wa wanaharakati wa makundi ya kiraia huko Baidoa, anasema kuwa aliyesababisha janga hili ndiye atakayewajibika, “ Tulishambuliwa” na isiwe ni kisingizio kwa kifo hiki. Aliiambia idhaa ya kisomali ya sauti ya America.

Anasema haki ya kujilinda haimanishi haki ya kuuwa raia. Anasema AMISOM inawajibika kwa usalama wa raia wa Somalia na hili limevuka mamlaka yao. Anasema tunataka uchunguzi kufanywa na fidia kulipwa kwa maisha yaliyopotea.

Katika taarifa iloandikwa kwenye mtandao wa twitter, AMISOM iliandika kuwa imepokea ripoti ya tuhuma za mauwaji ya raia katika mapambano baina ya vikosi vyake na Al Shabab katika eneo la Wardinle.

Taarifa hio imendelea kusema kuwa AMISOM inachukulia kwa dhati ripoti kama hizo na imeanza uchunguzi.

Takriban mwaka mmoja ulopita vikosi vya umoja wa Afrika vilikiri kuwa wanajeshi kutoka kitengo cha Uganda waliuwa raia 7 katika sherehe za harusi katika mji wa mwambao wa Marka baada ya shambulizi la bomu kwenye gari la kijeshi.

AMISOM iliomba msamaha kwa mauwaji ya raia hao 7.

XS
SM
MD
LG