Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 13:46

AU yatoa wito wa amani Burundi


mwenyekiti wa Umoja wa Afrika-AU, Nkosazana Dlamini-Zuma
mwenyekiti wa Umoja wa Afrika-AU, Nkosazana Dlamini-Zuma

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika-AU Nkosazane Dlamini Zuma aliwasihi wananchi wa Burundi kuepuka jambo lolote ambalo litavuruga amani iliyopo hivi sasa na wakati nchi hiyo inaelekea uchaguzi mkuu.

Bibi Zuma alitoa matamshi haya baada ya mkutano na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku mbili nchini humo huku kukiwa na khofu ya kuzuka ghasia katika upigaji kura kwenye uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika mwezi Juni.

Uchaguzi mkuu uliopita, Burundi Julai 23, 2010
Uchaguzi mkuu uliopita, Burundi Julai 23, 2010

Lengo la ziara yake ni kuiunga mkono Burundi wakati ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu wa urais, wabunge na serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika kutoka Mei 26 hadi Agosti 24 mwaka huu. Rais Pierre Nkurunzinza aliyepo madarakani hajatangaza rasmi kuwa atawania tena muhula mwingine na kumekuwepo na ongezeko la migawanyiko ndani ya chama chake cha CNDD-FDD juu ya kama anastahili kuwania tena kiti hicho.

Tangu jumatatu wiki hii zaidi ya wanachama waandamizi 70 wa chama hicho wakiwemo maafisa wa serikali, wabunge na maafisa wa serikali za mitaa wametia saini barua wakielezea upinzani wao juu ya bwana Nkurunzinza kuwania tena kiti hicho kwenye uchaguzi wa urais hapo mwezi Juni.

Akiongezea zaidi matamshi yake baada ya mkutano na bwana Nkurunzinza, mwenyekiti huyo wa AU alisema Burundi ilikuwa na mizozo yake na kwamba hivi sasa ni wakati kwa nchi hiyo kuendelea kuwa na amani. “Ni lazima iwe na amani kuelekea uchaguzi, lazima iwe na amani zaidi ya hapo. Na kila mtu kutoka serikalini kuelekea makundi ya kiraia lazima wafanye kila wawezalo kuendeleza amani au kutofanya jambo lolote ambalo litavuruga amani,” alisema bibi Zuma.

Kundi la kutetea haki za binadamu-Human Rights Watch
Kundi la kutetea haki za binadamu-Human Rights Watch

Akiwa nchini humo bibi.Zuma pia alifanya mikutano na wanachama wa vyama vya kisiasa, makundi ya kiraia yakiwemo makundi ya vijana na wanawake pamoja na viongozi wa kidini.

Bibi Zuma aliongeza kuwa “Ilikuwa fursa nzuri kwangu kuwa na majadiliano na Rais na kuzungumza naye kuhusu mlolongo wa masuala mbali mbali, kuhusu ukweli kwamba kunatakiwa uaminifu, hisia za usalama katika nchi na kila kitu lazima kifanyike ili kuhakikisha kwamba kuna usalama katika nchi kwenye kipindi hiki na baada ya hapo na pia kushauriana naye juu ya kile watu wengine wanavyosema kuhusu uchaguzi na kuhusu tume ya uchaguzi”.

Alisema wote walikubaliana kwamba Burundi inahitaji amani hivi sasa kuliko muda mwingine wowote ule ulioshuhudia.

Makundi ya haki za binadamu yalionya hatari za kuongezeka khofu na ghasia kabla ya uchaguzi.

Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika-AU aliitaka Burundi kufuata mkataba wa Amani uliotolewa mjini Arusha, Tanzania mwaka 2000 wa katiba na sheria za uchaguzi ili kuhakikisha uchaguzi wa Amani.

Mkataba wa Arusha na katiba unaruhusu rais kuchaguliwa mihula miwili yenye miaka mitano kila mmoja lakini haionekana kwenye mkataba, katiba inaelezea kwamba kidhibiti hiki kipo kwa rais aliyechaguliwa kwa muda kutokana na mizozo ya kisiasa.

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza

Wafuasi wa bwana Nkurunzinza wanasema kwamba rais huyo alichaguliwa kwa muda kutokana na mizozo ya kisiasa hapo mwaka 2010 na kwamba sio mihula miwili aliyohudumu madarakani tangu kuteuliwa kwake kwa mara ya kwanza kufuatia upigaji kura bungeni.

Wapinzani wake wanasisitiza kama anaamua kuwania tena, atakuwa anahudumu muhula wa tatu.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Bujumbura hapo jumatano Rais Nkurunzinza alisema fununu hizo juu ya kama atawania muhula mwingine au la zinatakiwa zisubiri hadi atakapotangaza kwa matamshi yake mwenyewe.

XS
SM
MD
LG