Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 16:49

AU yasema hadhi ya uangalizi ya Israel imesitishwa


Ramani ya Israel
Ramani ya Israel

Umoja wa Afrika Jumapili umesema kwamba hadhi ya uangalizi ya Israel kwenye Umoja huo imesitishwa na hivyo nchi hiyo haikualikwa kwenye mkutano wa AU mwishoni mwa juma, baada ya mzozo kuhusu kufukuzwa kwa mmoja wa wanadiplomasia wake wakuu.

Israel iliyokasirishwa na hatua hiyo imemshtumu hasimu wake mkuu Iran kwa kupanga njama ya kufukuzwa kwa mwanadiplomasia huyo siku ya ufunguzi wa mkutano wa AU Jumamosi kwa kusaidiwa na Algeria na Afrika Kusini.

Tukio hilo lilionyesha mzozo ndani ya Jumuia hiyo ya Afrika kuhusu uamuzi wa mwaka wa 2021 wa mkuu wa tume ya Umoja wa Afrika kuipa Israel hadhi ya kuwa mwangalizi.

Hatua hiyo ilipingwa na nchi wanachama zenye nguvu ikiwemo Afrika Kusini.

Mkutano wa AU wa mwaka jana ulisitisha mjadala kuhusu kuondoa hadhi hiyo na kuunda kamati ya wakuu wa nchi ili kushughulikia suala hilo.

“Hii inaamanisha kuwa hadhi hiyo imesitishwa hadi wakati kamati hii itakapochukua maamuzi, na kwa hivyo hatukualika maafisa wa Israel kwenye mkutano wetu,” Faki amewaambia waandishi wa habari Jumapili, akiongeza kuwa uchunguzi unaendeshwa.

XS
SM
MD
LG