Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 08, 2024 Local time: 14:31

AU yaendelea kuzitenga nchi nne za Afrika zinazotawaliwa na jeshi


Wakuu wa nchi za Afrika kwenye kikao cha 35 cha mkutano wa Umoja wa Afrika, Feb 5, 2022.
Wakuu wa nchi za Afrika kwenye kikao cha 35 cha mkutano wa Umoja wa Afrika, Feb 5, 2022.

Umoja wa Afrika Jumapili umesisitiza kuwa una sera ya kutovumilia mabadiliko yanayokiuka katiba, huku ukiendelea kusimamisha uanacahama wa nchi nne zinazotawaliwa na jeshi

Nchi za Sahel za Burkina Faso, Guinea na Mali vile vile Sudan ziliwekewa vikwazo na taasisi hiyo ya Afrika baada ya mapinduzi ya kijeshi katika miaka ya karibuni, lakini Umoja wa Afrika Jumapili umesema uko tayari kuzisaidia kurejea kwenye utawala wa kidemokrasia

“Mkutano umesisitiza kutovumilia kabisa mabadiliko yanayovunja katiba,” amesema Kamishna wa AU wa masuala ya kisiasa, amani na usalama, Bankole Adeoye.

“Tume iko tayari kuunga mkono nchi hizi wanachama kurejea katika utaratibu wa kikatiba, lengo ni kwamba demokrasia lazima iote mizizi na lazima iimarishwe na kulindwa,” aliuambia mkutano wa waandishi wa habari katika siku ya mwisho ya mkutano wa AU mjini Addis Ababa.

XS
SM
MD
LG