Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 20:04

Viongozi wa AU wakutana Rwanda


Rwanda AU Summit
Rwanda AU Summit

Mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika umeanza mjini Kigali Rwanda huku swala la mgogoro wa Sudan likiwa moja ya mambo makuu katika ajenda ya dharura.

Marais kadha wa Afrika wanahudhuria mkutano huo ambao pia unahudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon. Miongoni mwa ajenda za siku ya kwanza ya mkutano ni pamoja na maendeleo ya mpango wa ushirika wa maendeleo afrika – NEPAD.

Jumapili viongozi hao wa Afrika watakutana kujadili maswala kadha kuanzia mipango ya fedha hadi usalama na amani barani Afrika. Mkutano huo pia unatazamiwa kuchagua mwenyekiti mpya ya tume ya umoja wa Afrika kuchukua nafasi ya Nkosazana Dlamini-Zuma anayemaliza muda wake.

Mkutano huo unafanyika huku Sudan Kusini ikiwa katika mgogoro mkubwa uliozuka hivi majuzi baina ya rais na makamu rais wa nchi hiyo na kusababisha mamia ya watu kuuawa. Raia wengine wa nchi za kigeni wanaondoka nchini humo hivi sasa kuepuka ghasia.

XS
SM
MD
LG