Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 13:13

AU yasitisha uanachama wa Guinea-Bissau


Wananchi wakitembea nje ya jengo la bunge nchini Guinea-Bissau, March 19,2012
Wananchi wakitembea nje ya jengo la bunge nchini Guinea-Bissau, March 19,2012

Wanasiasa nchini Guinea-Bissau watakiwa kuepuka kujihusisha na viongozi waliofanya mapinduzi nchini humo

Umoja wa Afrika umesitisha uanachama wa nchi ya Guinea-Bissau kufuatia mapinduzi ya wiki iliyopita yaliyofanywa na jeshi.

Baraza la Usalama na Amani la Umoja wa Afrika lilisema Jumanne kwamba Guinea-Bissau inasimamishwa kwa muda kushiriki katika kazi zake zote hadi kurudishwa kwa utawala wa kikatiba katika taifa hilo lililopo Afrika magharibi.

Katika taarifa yake, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Jean Ping, alikataa juhudi zilizofanywa na viongozi waliofanya mapinduzi za kuweka baraza la muda la kitaifa.

Alisema viongozi waliofanya mapinduzi wanakiuka katiba na aliwasihi wanasiasa nchini Guinea-Bissau kuepuka kujihusisha katika kile alichokiita njia ya kutaka kuhalalisha mapinduzi hayo.

Alisema pia viongozi waliofanya mapinduzi wanajaribu kuzima taratibu za uchaguzi zinazoendelea.

Uchaguzi wa marudio ulipangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu kuziba nafasi ya marehemu Rais Malam Bacai Sanha, ambaye alifariki mwezi Januari baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Mapema Jumanne Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi-ECOWAS ilisema viongozi waliofanya mapinduzi wamekubali dai lao la kurejesha amri ya katiba, kufuatia mazungumzo kati ya pande hizo mbili. Hakukuwa na majibu yeyote kutoka kwa baraza la kijeshi.

Rais wa kamisheni wa ECOWAS, Desire Kadre Ouadraogo alisema kundi pia lilidai kuachiwa kwa wafungwa.

Wanajeshi waliwakamata Rais wa muda, Raimundo Pereira na Waziri Mkuu wa zamani, Carlos Gomes Junior, wakati jeshi lilipochukua madaraka, alhamis iliyopita.

Bwana Gomes alikuwa mgombea anayeongoza katika duru ya marudio ya kinyang’anyiro cha nafasi ya kiti cha rais ambacho kilipangwa kufanyika April 29. Mpinzani wake Kumba Yala, ni rais wa zamani ambaye alikuwa na ushirika wa karibu na jeshi.

Bwana Gomes alishinda duru ya kwanza ya uchaguzi lakini alipungukiwa na kura zilizohitajika kumpatia ushindi.

XS
SM
MD
LG