Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 05:23

AU:Hatumtambui Laurent Gbagbo

Alasssane Ouattara, kiongozi anayekubalika na AU, UN na jumuiya ya kimataifa kwa Ivory Coast
Alasssane Ouattara, kiongozi anayekubalika na AU, UN na jumuiya ya kimataifa kwa Ivory Coast

Umoja wa Afrika imesitisha uanachama wa Ivory Coast, kwa sababu rais Laurent Gbagbo amekataa kukabidhi madaraka baada ya uchaguzi wa mwezi uliopita.

Umoja wa Afrika imesitisha uanachama wa Ivory Coast, kwa sababu rais Laurent Gbagbo amekataa kukabidhi madaraka baada ya uchaguzi wa mwezi uliopita.

Kamishna wa ulinzi na amani wa Umoja wa Afrika, Ramtane Lamamra, alisema Alhamisi kwamba Ivory Coast imesimamishwa kushiriki shughuli zote za Umoja wa Afrika hadi rais aliyechaguliwa kidemokrasia, Alassane Ouattara, akabidhiwe madaraka.

Tume ya uchaguzi nchini Ivory Coast, ilimtaja bwana Ouattara mshindi wa uchaguzi wa mwezi uliopita, matamshi yaliyoungwa mkono na Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa.

Lakini bwana Gbagbo anaendelea kudhibiti jeshi na televisheni ya taifa na haonyeshi dalili za kuondoka madarakani. Marekani ilisema Alhamisi huenda ikamuwekea vikwazo bwana Gbagbo na watu wengine walio karibu naye kama atashindwa kujiuzulu.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani anasema Rais wa Marekani, Barack Obama alituma barua kwa bwana Gbagbo ikionya kwamba kama akifanya maamuzi ambayo si sahihi huenda yatapelekea kutengwa kwa Ivory Coast na serikali yake.

XS
SM
MD
LG