Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 21:58

AU yamaliza mkutano bila uamuzi wa Burundi


Ukumbi wa mkutano wakati wa kufunga Jumapili, Addis Ababa, Jan. 31, 2016.
Ukumbi wa mkutano wakati wa kufunga Jumapili, Addis Ababa, Jan. 31, 2016.

Na Martha van der Wolf

ADDIS ABABA - Umoja wa Afrika ulimaliza mkutano wake wa wakuu wa nchi Jumapili, bila uamuzi wa hatua kuhusu swala la Burundi.

Umoja wa Afrika haukuweza kukusanya kura za kutosha katika mkutano huo kupeleka wanajeshi wa kulinda amani Burundi, bila idhini ya Burundi yenyewe, licha ya uamuzi kutoka katika Baraza la Amani na Usalama la AU mwezi Disemba kupelekea majeshi kusitisha umwagaji damu.

Kamishna na Baraza hilo, Smail Chergui alisema AU itatuma ujumbe wa ngazi ya juu Burundi kuendelea na mashauriano kuhusu swala hilo.

Anasema kama Burundi itakubali kupelekwa kwa jeshi hilo litatilia mkazo kuwapokonya silaha wanamgambo, kulinda raia, kuwezesha shughuli za wafuatiliaji wa haki za binadamu, na kukusanya silaha ambazo zinazunguka kinyume cha sheria.

Msimamo wa Burundi

Waziri wa mambo ya nje wa Burundi Alan Nyamitwe alisema mkutano huo ulimalizika kwa makubaliano ya wazi kuwa ujumbe utakaokwenda Burundi hautahusu upelekaji wa majeshi nchini humo.

"Kwa vile serikali imeonyesha mara chungu nzima kuwa hatutaki jeshi hilo, na iko wazi, ujumbe huo hautajihusisha na swala la jeshi, kwa sababu tumeeleza msimamo wetu wazi mara nyingi," alisema.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon aliwaambia waandishi wa habari "kimsingi ni swala la Umoja wa Afrika, kwa kushauriana na serikali ya Burundi."

Naibu Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Linda Thomas-Greenfield anasema kupeleka walinzi wa amani itakuwa katika maslahi ya watu wa Burundi.

Rais wa Chad Idriss Deby alifunga mkutano huo Jumapili kwa wito wa ushirikiano zaidfi katika kupambana na ugaidi, kuheshimu hadj za binadamu na kuwafanya vijana wa Afrika wasikilimbie Ulaya kwa njia zisizo halali.

XS
SM
MD
LG