Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:11

Atlantis yatua kwa mara ya mwisho


Atlantis ikitua katiika kituo cha safari za anga cha Kennedy Space Center huko Cape Canaveral, Florida, July 21, 2011
Atlantis ikitua katiika kituo cha safari za anga cha Kennedy Space Center huko Cape Canaveral, Florida, July 21, 2011

Kurejea kwa Atlantis kunakamilisha safari za anga za Marekani baada ya miaka 30

Chombo cha anga Atlantis kimetua salama Alhamisi asubuhi katika kituo cha anga cha Kennedy huko Florida na kumaliza safari za anga za Marekani baada ya miaka 30.

Kundi kubwa la watu lilishangilia kutua kwa chombo hicho. Safari ya siku 13 ya Atlantis angani ilikuwa ya 33 baada ya kutumika kwa miaka 26.

Wanaanga wa chombo hicho waliondoka katika kituo cha kimataifa angani Jumanne baada ya siku nane za kazi za kupeleka mahitaji muhimu katika kituo hicho na kubeba takataka na vifaa vilivyotumika.

Atlantis na vyombo vingine vilivyotumika kwa safari za anga vitastaafishwa na kuwekwa katika makumbusho ya kitaifa.

Ingawa NASA, idara ya safari za anga ya Marekani, ina mipango ya muda mrefu ya kuhudumia kituo cha kimataifa angani, haina mpango wa kupeleka wanaanga juu kwa miaka kadha ijayo.

XS
SM
MD
LG